Mhubiri wa Kiislamu nchini Uganda, Sheikh Muhammad Kirevu ameuawa kwa kupigwa risasi na vikosi vya usalama nchini humo baada ya kutuhumiwa kufanya kazi na kundi la watu wenye silaha wanaohusishwa na milipuko miwili ya kujitoa mhanga iliyotokea Jumanne katika mji mkuu wa Kampala.
Maafisa nchini humo wamesema shekhe Kirevu alikuwa amewaandikisha vijana kujiunga na makundi ya kigaidi .
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Fred Enanga amesema msako unaendelea kumtafuta imamu mwingine, Sheikh Suleiman Nsubuga ambaye anatuhumiwa kutoa mafunzo kwa magaidi.
Takriban watu wanne waliuawa na washambuliaji waliokuwa kwenye pikipiki ambao walijilipua mjini humo.