Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina Emmanuel Issack amekwama ardhini kwa zaidi ya siku saba baada ya kifusi cha mabaki ya machimbo ya dhahabu kushuka na kuziba upenyo wa shimo walilokuwa wakitumia kuingilia kwa shughuli za machimbo katika mgodi wa Mhalu, kitongoji cha Nyamatongo wilayani Kwimba mkoani Mwanza.
Katika ajali hiyo iliyotokea usiku wa tarehe 7, watu nane wamenusurika baada ya kukimbilia katika mashimo jirani ndani ya mgodi huo na kuokolewa baadaye na wachimbaji wengine waliokuwa nje mara tu walipopokea ishara kupitia waya unaotumika kupanda na kushuka katika mashimo hayo.
Waziri wa madini Mh. Dotto Biteko amefika katika mgodi huo kuwafariji ndugu na wachimbaji huku akisisitiza juhudi zaidi kufanyika ili kumuokoa kijana huyo.