Mkutano Mkuu wa 41 wa UNESCO umeipitisha tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa Siku ya Kiswahili Duniani, azimio hilo limepitishwa na Nchi zote Wanachama wa UNESCO bila kupingwa leo November 23, 2021, Paris nchini Ufaransa.
Hatua hii inakifanya Kiswahili kuwa lugha ya kwanza Afrika kutambulika na Umoja wa Mataifa na siku maalumu ya kuadhimishwa.
“Hizi ni miongoni mwa jitihada za Serikali ya Tanzania katika kukikuza Kiswahili na kuenzi urithi tulioachiwa na Muasisi wa Taifa letu Mwl. J.K Nyerere” ——— Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa