Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa amemtaka Mkandarasi anayejenga chuo cha VETA Wilayani Chunya Mkoani Mbeya kuhakikisha anafanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha ujenzi wa chuo hicho kwa muda uliokusudiwa na Wana-Chunya waanze kupata mafunzo kuanzia mwezi Februari 2022,
Ametoa agizo hilo Novemba 29, 2021 wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Chunya, Mkoani Mbeya.
Amesema kuwa malengo ya Rais Samia ni kuhakikisha kila makao makuu ya mikoa kunajengwa chuo kikubwa cha VETA
Chuo cha VETA cha Wilaya ya Chunya kitakachogharimu shilingi bilioni 1.6 kinajengwa katika kata ya Mbugani,kinatarajiwa kuhudumia jumla ya kata 20 zenye wakazi wasiopungua 211,039.
Pia, Waziri Mkuu ameziagiza Halmashauri za Wilaya kuhakikisha wanalinda vyanzo vya maji na wawahamishe wananchi kupanda miti na kushirikiana nao kupitia kamati zao za mazingira ili walinde vyanzo hivyo kuanzia ngazi ya kijiji kwa manufaa yao.