Serikali ya Tanzania imesema kutokana na juhudi za Serikali za kuendeleza na kuimarisha utangazaji wa vivutio vya utalii nchini, idadi ya Watalii wanaoingia nchini kutoka katika nchi mbalimbali Duniani imeongezeka kutoka 9,847 Mwaka 1960 hadi kufikia watalii 1,527,230 Mwaka 2019.
Wizara hiyo imetoa taarifa ya mafanikio na maendeleo ya Wizara hiyo katika kipindi cha miaka 60 ya Uhuru ambapo imesema kumekuwepo na ongezeko la mapato yatokanayo na watalii, kwa mfano mwaka 1995 mapato yalikuwa Dola za Marekani milioni 259.44 ambapo yaliendelea kuongezeka hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 2.6 mwaka 2019 kabla ya Ugonjwa wa UVIKO-19.
“Kutokana na jitihada za Serikali katika kukabliliana na ugonjwa wa UVIKO-19 idadi ya watalii imeanza kuongezeka kutoka watalii 620.867 mwaka 2020 hadi kufikia 716,169 mwezi Oktoba 2021”