Tunarudi tulikotoka?, Serikali nchini Zimbabwe imetangaza kurejesha tena marufuku ya kutotoka nje (lockdown) na Wasafiri wote watapaswa kukaa Karantini, hatua hii inakuja wakati huu ambapo kuna ongezeko la maambukizi ya Covid na Zimbabwe inasema inafanya hivyo ili kuzuia kuenea kwa aina mpya ya kirusi kipya cha Omicron.
Zimbabwe imeripoti maambukizi ya Covid 130,000 na vifo 4,700 tangu kuanza kwa Ugonjwa mwaka jana na imesema kuna hofu pia ya wimbi la nne lakini Wananchi wanasema hali ya kiuchumi itakuwa mbaya kutokana na masharti hayo mapya.
Rais Emmerson Mnangagwa ametangaza marufuku ya kutotoka nje kuanzia saa tatu usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi.