Kiongozi aliyepinduliwa nchini Myanmar, Aung San Suu Kyi amehukumiw akifungo cha miaka minne gerezani sambamba na mshirika wake na rais wa zamani wa nchi hiyo Win Myint.
Wawili hao wamekutwa na hatia katika mshtaka manne kati ya mashtaka 11 yanayowakabili.
Suu Kyi na Myint wamekutwa na hatia katika mashtaka ya kuvunja amri ya kujikinga dhidi ya maambukizo ya Covid-19 kwa kuwapungia mkono wafuasi wao wakati wa kampeni za uchaguzi huku wakiwa wamevaa barakoa.
Pia wawili hao wamekutwa na hatia katika shtaka la uchochezi kwa kutolewa taarifa na chama chao ya kupinga mapinduzi ya kijeshi nchini humo kufuatia hatua ya kuzuiwa nyumbani kwa viongozi wa chama chao cha National League for Democracy (NLD).
Tangu mwezi Februari, Suu Kyi amekuwa kwenye kizuizi cha nyumbani na serikali yake kupinduliwa na jeshi la nchi hiyo.