Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James amesema bado Jeshi la Polisi, Zimamoto na Vyombo vingine vya Ulinzi mpaka sasa vipo katika eneo la Goba ambako ghorofa limeporomoka na kuua Watu wanne na kujeruhi wengine 17, Kheri amessema wapo hapo ili kuhakikisha kama waliojeruhiwa ni Watu 17 tu ama kuna ziada.
“Serikali imechukua hatua ya kuhakikisha waliojeruhiwa wanapatiwa matibabu na maiti zote tumezipeleka Mloganzila, tunawasihi na kuwasisitiza Wananchi kwamba wasisogee jirani na eneo hili kwa sana, kwasababu jengo hili bado limekaa katika mkao wa kuanguka zaidi na zaidi” “——— DC wa Ubungo, Kheri James