Polisi Mkoa wa Kagera wamethibitisha kutokea kwa kifo cha Mkulima mmoja aliyepigwa risasi wakati wa vurugu za Wakulima na Walinzi wa Wawekezaji wa mifugo katika eneo la Rutoro.
RPC Awadhi Juma Haji amefika eneo la tukio na kueleza kuwa baadhi ya Wakulima wakiwa na silaha za jadi walivamia kwenye kitalu cha Mfugaji wa eneo la Rutoro na kuanza kushambuliana na Walinzi ambao walikuwa na bunduki.