Ayo TV inakukutanisha na historia ya hifadhi ya Taifa ya Nyerere ambayohapo awali ilijulikana kama Pori la Akiba la Selous.
Inaelezwa kuwa Selous ni jina la mwindaji ambae alikuwa raia wa Uingereza aliepigana vita kuu ya kwanza ya dunia katika pori hilo na aliuwa na ndipo pori hilo likapewa jina lake.
Rais wa awamu ya Tano, Hayati John Magufuli akalibadilisha na kuliita Hifadhi ya Taifa ya Nyerere.