Serikali imeokoa takribani Shilingi Bilion 4 baada ya kuamua kutekeleza mradi wa maji Kirando kwa Mfumo wa Force Account kwa kutumia Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maji ambazo ni Mamlaka ya Maji Sumbawanga na Wakala wa Maji Vijijini RUWASA.
Mradi huo ulitakiwa kutekelezwa kwa Bilion 7.7 na sasa utatekelezwa mpaka mwisho kwa Bilion 3.1
Mradi wa Maji Kirando ambao unatumia chanzo cha Ziwa Tanganyika umekamilika kwa Wastani wa Asilimia 95 na umeanza kuwanufaisha Wananchi wa Vijiji 7 vya Wilaya ya Nkasi Mkoa wa Rukwa.
Kabla ya mradi kuanza kutoa huduma ya maji, Wananchi wa Kirando walikuwa wanatumia maji ambayo sio safi wala salama katika madimbwi ya maji lakini sasa wamepata ukombozi kupitia mradi huu ambao utawanufaisha Wakazi 74,341, amesema Waziri wa maji Jumaa Aweso