Mtawala wa Dubai Sheikh Mohammed Bin Rashid Al Makhtoum (72) ameamriwa na Mahakama ya Jijini London kumlipa mkewe wa zamani binti Mfalme Haya Bint Hussein (47) dola za Kimarekani Milioni 728.
Kesi hii imekuwa ni moja kati ya kesi za gharama kubwa kuliko kesi zote za usuluhishi wa talaka zilizowahi kusimamiwa na Mahakama ya Uingereza.
Pesa hizo zitatumika kugharamia ulinzi wa Binti Mfalme huyo kwa maisha yake yote pamoja na gharama zote za kuwalea watoto wao wawili Jalila (14) na Zayed (9) .
Sheikh Mohammed atatakiwa kulipa takribani dola za kimarekani milioni 333 kwa mkupuo ndani ya miezi 3 ijayo na kuendelea kulipa pesa zingine kwa kila mwaka.