Vilio na Simanzi vimetawala wakati wa ibada ya kumuaga Mwanafunzi ambaye amehitimu katika Chuo Cha SUA mkoani Morogoro, Magreth Mashuwe aliyeuwawa na watu wasiojulikana katika mashamba ya Chuo hicho hivi karibuni.
Ibada hiyo imefanyika katika viwanja wa Mochwari ya Hospitali ya Rufaa mkoa Morogoro ambayo imehudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki.
Akizungumza mara baada ya ibada hiyo, Dada wa marehemu Liliani Mashuwe amesema mazishi yanatarajia kufanyika katika Kijiji cha Shimbikati kata ya Mkuu, wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro Disemba 23, 2021.
Anasema wao kama familia wanaziachia mamlaka husika kufuatilia tukio hilo ili kuwabaini waliohusika.
Kwa upande wake Mchungaji wa kanisa la Tanzania Assemble of God (TAG) Dismas Kimario amewataka ndugu wa marehemu kumshukuru Mungu kila jambo kama maandiko ya Biblia takatifu yanavyosema.