Madakatari nchini Israel Jumatatu wameanza kutoa chanjo ya nne ya covid 19 kwa watu wake ikiwa kama sehemu ya majaribio kuona kama chanjo ya ziada itaongeza kinga ya mwili dhidi ya maambukizi ya corona.
Majaribio hayo yanawahusisha takriban wafanyakazi 150 kutoka kituo cha afya cha Sheba karibu na Tel Aviv, siku chache baada ya jopo la wataalamu wa afya kupendekeza chanjo ya nne ya Pfizer kwa watu wenye umri miaka 60 au zaidi, pamoja na wale wenye matatizo ya kiafya.
Hata hivyo ni lazima mkuruguenzi katika wizara ya afya Nachman Ash aidhinishe pendekezo hilo. Israel ni miongoni mwa mataifa yanayoongoza katika utoaji wa chanjo kwa watu wake ikiwemo ile ya booster ingawa kasi imepunguka katika wiki za karibuni huku kukiwa na wimbi la tano la maambukizi ya covid kutokana na aina mpya ya virusi vya omicron.
Virusi hivyo vinavyo semekana kusambaa kwa haraka vimepelekea baadhi ya mataifa kufunga shughuli za kawaida pamoja na safari za ndege kusitishwa kote ulimwenguni. Virusi hivyo viligundulika kwa mara ya kwanza mwezi iuiopita kwenye baadhi ya mataifa ya kusini mwa Afrika.