Maafisa wa afya nchini Marekani wamefupisha muda uliopendekezwa wa kujitenga kwa Wamarekani wasio na dalili za COVID-19 hadi siku tano kutoka mwongozo wa awali wa siku 10.
Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa-CDC pia vilisema watu ambao wamepimwa na kukutwa na virusi baada ya kujitenga wanapaswa kufuata siku tano za kuvaa barakoa wanapokuwa karibu na wengine.
Omicron inachukua asilimia 73 ya maambukizi ya corona kote nchini Marekani, CDC ilisema wiki iliyopita.
Maambukizi yanaongezeka kati ya idadi ya watu waliopewa chanjo kamili, pamoja na wale ambao wamepewa chanjo ya tatu ya nyongeza. Hata hivyo, Omicron inaonekana kusababisha dalili zisizo kali zaidi kwa watu hao, ambao baadhi yao hawana dalili zozote.