Madaktari wa Baltimore Marekani wamefanikiwa kuupandikiza moyo wa Nguruwe kwa Binadamu ambaye amekua akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo na kutishia uhai wake lakini sasa kapata tumaini jipya baada ya kuwekewa moyo wa Nguruwe aliyebadilishwa vinasaba.
Ni kupandikiza kwa kwanza kwa mafanikio ya moyo wa nguruwe ndani ya mwili wa Mwanadamu ambapo upasuaji huo uliochukua dakika 480 (saa nane) ulifanyika Baltimore siku ya Ijumaa na sasa Mgonjwa mwenyewe aitwae David Bennett Sr. wa Maryland anaendelea vizuri kiafya, wamesema Madaktari wa upasuaji katika Chuo Kikuu cha Maryland Medical Center.
“Moyo huo wa Nguruwe unafanya kazi kama kawaida, tumefurahi lakini hatujui kesho utatuletea nini kwani hili halijawahi kufanywa kwa Binadamu”
Habari hii imekuja ikiwa ni miezi miwili tu imepita toka Madaktari wa New York Marekani watangaze kufanikiwa kupandikiza figo ya Nguruwe kwa Binadamu.
MUSUKUMA “WALIOCHUKUA FOMU USPIKA WAJITOE, UNAUNDAJE SUKUMA GANG MIMI SIPO”