Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watoto wa Kitanzania kujiwekea malengo na kusoma kwa bidii ili kupata maarifa yatakayolisaidia taifa kupata maendeleo huku Serikali ikiendelea kuweka mazingira bora ya kujifunzia.
Waziri Majaliwa ametoa rai hiyo leo Jumatatu, Januari 24, 2022 mara baada ya kukagua ujenzi wa madarasa katika Shule ya Sekondari Gehandu na Nowu zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.
Aidha Waziri Mkuu amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Elimu kufanya mapitio ya sera ili kuifanya sekta hiyo kuendelea kufanya vizuri zaidi.
Waziri Mkuu ameziagiza Halmashauri zote nchini kuweka mpango wa ujenzi wa mabweni kupitia mapato ya halmashauri na iwapo itakapotokea Serikali imeweka mpango wa ujenzi wa mabweni watatumia fedha zao kama ujazilizi kwenye fedha hiyo
“Anzeni ma watoto wanaotembea umbali mrefu, hili linawezekana mkiweka mpango mzuri”
Aidha, amewakumbusha watumishi wa umma kutambua kuwa wanajukumu kubwa la kuwatumikia watanzania na kutekeleza maelekezo ya ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.
Ujenzi wa madarasa hayo unatokana na fedha za mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19.