Mkuu wa Wilaya Hashim Shaibu Mgandilwa amefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo pamoja na masoko yaliyopo mkoani Tanga.
Aidha katika ziara yake ametoa wito kwa wafanyabiashara kuwa makini ndani ya masoko yao baada ya tuharuki iliyoibuka ya kuungua kwa masoko nchini.
‘Ningependa kuwaomba wafanyabiashara wote wa Masoko tuwe na umakini sana, tunaona kwasasa kuna taharuki ya kuugua kwa masoko nawaomba sana wakina Mama hususani Mamantilie wasiache wamebandika Maharage na vitu vingine ili visiwe chanzo katika masoko yetu’– DC wa Tanga
Pia amewasisitiza wanachi wanaopokea mikopo kuhakikisha wanarudisha marejesho ya mikopo kwa wakati hata na kuwaomba wananchi kulinda na kutunza miundombinu ya miradi inayoletwa katika maeneo yao.
HALIMA MDEE AIBUKA NA HOJA YA MIKOPO YA NJE “TUIPUNGUZIE SERIKALI MZIGO”