Shirikisho la Wamachinga Tanzania (SHIUMA) wamekutana Dar es Salaam na kupewa mafunzo ya Elimu ya fedha iliyoendeshwa na benki ya CRDB.
Akizungumza mbele ya waandishi Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Umoja wa Wamachinga mkoa wa Dar es salaam, Steven Lusinde
‘Tumekuja kupata Elimu ya kifedha namna gani tunaweza kuendesha saccos hii ambayo ndio saccoss ya kihistoria, saccoss imeanzia Wamachinga wa Dar es Salaam, ndio maana tumealika Wamachinga wa mikoani waje kujifunza’- Steven Lusinde
‘Malengo yetu Saccos yetu iendee nchin nzima na ndio maana tumealika mikoa 15 wapo hapa kuhakikisha wanajifunza kupitia CRDB kuhakikisha namna gani wanaweza kuendesha hii saccos’- Steven Lusinde
‘Saccoss hii ni kupoza machungu ya muda mrefu mnaweza mkawa mnafahamu kwamba tokea Uhuru wamachinga hawajawahi kupata huru wa namna hii kwahiyo Serikali ya Awamu ya tano na Awamu ya sita imekuja kukazia huru wa mmachinga kufanya biashara ndani ya utaratibu na kujiwezesha wenyewe kwa wenyewe’- Steven Lusinde
Mafunzo haya yamehudhuriwa na Shirikisho la Umoja wa Wamachinga mkoa wa Dar es salaam (Machinga Saccos) na baadhi ya wawakilishi wa wafanyabiashara hao kutoka Mikoa yote Tanzania ikiwa ni mwendelezo wa ushirikiano tulionao kati ya Benki yetu na wafanyabiashara wadogo (Wamachinga).
NANDY KAFUNGUKA BILLNASS KUMVALISHA PETE ‘WASHENGA WALIPENDEKEZA MAHARI YA MILIONI 10’