Mfanyabiashara Azim Dewji, amewataka Wachezaji wa timu ya Simba kutobweteka na matokeo wanayoyapata ikiwemo ya michuano ya Shirikisho la Klabu Bingwa Afrika.
Azim Dewji ameyasema hayo leo mbele ya Waandishi wa Habari, ambapo amesema timu hiyo kwa sasa inaenda kwa mwendo mdogo ila kadri siku zinavyokwenda inafanya vizuri.