Mke wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa madini mkoani Arusha, marehemu Erasto Msuya, Miriam Mrita amekiri kuhusu katika mauaji ya wifi yake, Aneth Msuya kupitia maelezo ya onyo yalisomwa na shahidi mahakamani.
Mbali na Miriam ambaye ni mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo namba 103 ya mwaka 2018 inayosikilizwa na Jaji Edwin Kakolaki, mshitakiwa mwingine ni mfanyabiashara Revocatus Myella.