Baada ya Polisi kumkamata na kumshikilia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la CHADEMA Hashimu Juma leo muda mfupi baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) kumuondolea mashtaka na kuachiwa na Mahakama, Wakili wake amesema hadi sasa hawajajua sababu za kukamatwa tena kwa Kiongozi huyo.
“Hatujajua sababu za kukamatwa tena ila amekamatwa baada ya DPP kumuondolea mashtaka ya uchochezi, tunafatilia suala la dhamana katika Kituo cha Polisi cha Kati”
Hashimu Juma alifikishwa kwa mara ya kwanza Mahakamani hapo Oktoba 7, 2021 kwa mashtaka ya uchochezi ikiwemo kudaiwa kuchapisha taarifa za uongo na kuisambaza Youtube.
RAIS SAMIA AMJIBU ASKOFU NIWEMUGIZI “HIYO SI TABIA YANGU,NAJITAHIDI KUJISHUSHA”