Wakati mzozo wa Ukraine na Urusi ukiendelea kushika kasi, Korea Kaskazini imerusha kombora linalodhaniwa kuwa la masafa marefu kuelekea Baharini katika muendelezo wa majaribio yake ya silaha.
Majaribio hayo ni ya nane kwa mwaka huu pekee huku baadhi ya Watalaamu wakisema kwamba Korea Kaskazini inajaribu kukamilisha teknolojia yake ya silaha na kuishinikiza Marekani kutoa makubaliano kama vile kuiondolea vikwazo.
Wakuu wa vikosi vyote vya majeshi nchini Korea Kusini, wamethibitisha juu ya Korea Kaskazini kurusha makombora lakini hawakutoa maelezo zaidi, bado Korea Kaskazini haijato kauli kuhusu mzozo wa Ukraine na Urusi.
Kwa habari zaidi unaweza ukatazama hii video tumekuandalia taarifa kamili.