Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeweka rekodi katika ujenzi wa Mkongo Taifa, ambapo kwa mwaka mmoja pekee Wizara imefanikiwa kujenga kilometa 4442 za Mkongo wa Taifa.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Kundo Mathew (Mb), alipotembelea Ofisi za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Singida.
“Zamani wakati mkongo unaanza kujengwa, utekelezaji wake ulianza kutekelezwa na kampuni za nje, nakumbuka enzi hizo nikiwa mtaalamu katika utumishi wangu wa umma”
“Kulikuwa na kampuni ya CITCC wakati huo ambayo ndio ilitekeleza ujenzi huo kuanzia mwaka 2009 lakini mpaka kufikia mwaka 2016 tulikuwa tumeshajenga takribani kilometa 7,560”-amesema Naibu Waziri Mhe. Mhandisi Kundo Mathew.
Amesema kutokana na vijana wengi kusomea kazi hiyo na watalaamu wengi wa ndani ya nchi wakafanikiwa kujenga kilometa 350 na kampuni ya ndani ya nchi Pamoja na kilometa nyingine 400 ambazo pia zimejengwa na kampuni ya ndani.
“Hapo utaona katika miaka kumi na kitu za ujenzi wa kilometa 8,000 sisi tunaenda kujenga kilometa 4442 ndani ya mwaka mmoja wa fedha, haya ndio Mapinduzi makubwa ya Sekta ya Mawasiliano”-ameongeza Mheshimiwa Mhandisi Kundo Mathew.
Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Kyaratu amesema kitendo cha Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kushirikiana na TANESCO kutasaidia kuokoa fedha kutokana na miundombinu hiyo hiyo ya Tanesco kutumika kwenye mawasiliano.
Katika ziara hiyo Naibu Waziri Mheshimiwa Kundo Mathewa aliambatana na Mbunge wa Singida Kaskazini Ramadhani Ighondo, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Paskas Muragiri.
WANANCHI WA UKRAINE WAKABIDHIWA SILAHA, WAINGIA NAZO MITAANI KUWAKABILIA URUSI