Ni habari za Kimataifa, kuhusu mvutano baina ya Ukraine na Urusi, ambapo wananchi wa Ukraine wametii agizo la Rais wao na kuingia katika uwanja wa vita kupambana na vikosi vya Jeshi la Urusi.
Itakumbukwa kwamba hivi karibuni baada ya Urusi kuishambulia Ukraine, Rais wa Ukraine aliwaomba wananchi washirikiane katika Mapambano na wasiojua kupigana na kushika bunduki basi watafundishwa.
Kitakwimu Ukraine ina raia wapatao Mil.44.13, huku ikiwa na Wanajeshi wapatao Laki Mbili na Nusu, ikiwa ni idadi ndogo ukilinganisha na Urusi yenye wanajeshi takribani Laki Tisa.
Ikiwa ni siku chache tangu mamia ya wakazi wa nchi kukubaliana na Rais wao, hatimaye raia wameingia vitani baada ya kupata mafunzo ya muda mfupi.
Hata hivyo si raia tu bali hata Rais mwenyewe ameingia vitani, pamoja na Rais mstaafu wa nchi hiyo Poroshenko ili kuhakikisha wanailinda nchi yao.
Kwa taarifa zaidi Ayo TV & Millardayo.com imekuandalia stori kamili unaweza ukabonyeza play kufahamu zaidi.