Rais wa Marekani Joe Biden ameliambia bunge la Congress kwamba rais wa Urusi Vladimir Putin alikosea kimtazamo kuhusu namna nchi za Magharibi zingejibu mapigo wakati alipoivamia Ukraine.
Akizungumza katika bunge hilo alisema “Niseme wazi, vikosi vyetu havishiriki na hatujishughulishi na migogoro na vikosi vya Urusi huko Ukraine. Vikosi vyetu haviendi Ulaya kupigana na Ukraine, bali kutetea washirika wetu wa Nato endapo Putin ataamua kuendelea kuelekea magharibi.”
“Kwa Wamarekani wote, nitakuwa mkweli kwenu, kama nilivyoahidi kuwa Dikteta wa Urusi anayevamia nchi ya kigeni amezunguka ulimwengu. Nachukua hatua madhubuti kuhakikisha maumivu ya vikwazo yanalengwa kwa uchumi wa Urusi. Na tutatumia kila zana tuliyo nayo kulinda biashara na watumiaji wa Marekani.”
Biden akilihutubia bunge hilo alisema ” Putin alidhani nchi za Magharibi na NATO zisingechukua hatua. Na, alidhani angeweza kutugawanya hapa nyumbani.
“Putin alikosea. Tulikuwa tayari.” Aidha Biden alitangaza kuwa Marekani itapiga marufuku ndege za Urusi katika anga yake, kama zilivyofanya mamlaka za Canada na Ulaya.
Ayo TV & Millardayo.com imekuandalia hapa stori kamili unaweza ukabonyeza play kufahamu zaidi.
RAIS WA UKRAINE AONGEA BAADA YA URUSI KURUSHA KOMBORA “HAKUNA ATAKAYESAMEHE,TUNA NGUVU, HAIJALISHI’