Wanajeshi 498 wa Urusi wameuawa na karibu 1,600 kujeruhiwa wakati wa mapigano yanayoendelea dhidi ya Ukraine, jeshi la Urusi lilidai Jumatano.
Wizara ya Ulinzi ilikanusha ripoti kwamba kumekuwa na “namba isiyohesabika” yawa athrika, ikitaja madai hayo kama upotoshaji wa makusudi unaotoka kwa adui.
Kulingana na makadirio ya jeshi la Urusi, vitengo vya jeshi la Ukraine na wanamgambo wa mrengo wa kulia wameripotiwa kupoteza takriban wanajeshi 2,870, huku wengine 3,700 wamepata majeraha kadhaa. Baadhi ya wanajeshi 572 wa Ukraine wamechukuliwa mateka, wizara iliongeza.
Vikosi vya Urusi vilivyohusika katika shambulio hilo vinajumuisha askari wa kitaalam pekee, jeshi limesema, na kukanusha madai kwamba jeshi la uvamizi lilikuwa na “makuruta”.
Takwimu rasmi za majeruhi zilizotangazwa na Moscow zinatofautiana kwa kiasi kikubwa na madai yaliyotolewa na Kiev, ambayo ilisema zaidi ya wanajeshi 5,800 wa Urusi wameangamia tangu uvamizi huo uanze.