Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabir Bakari amesema hadi takwimu za mwezi January mwaka huu ni Asilimia 27 pekee ya Watanzania ndio wanamiliki Simu janja (Smartphone) na kusema malengo ya Serikali ni kuhakikisha Watumiaji wa Smartphone wanafikia 100%.
Dr. Jabir ameiambia AyoTV na millardayo.com kwamba gharama za kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine zimeshuka kutoka Tsh. 2. 6 kwa dakika mwaka 2021 hadi kufikia Tsh. 2.0 kwa dakika kwa mwaka 2022. Dr. Jabir ametoa pia takwimu kutoka kwenye tafiti mbalimbali ambazo zinaonesha Kati ya Nchi 155 Ulimwenguni, Tanzania inashika nafasi ya 21 kwa unafuu wa gharama za kununua GB 1, pia Tanzania inashika nafasi ya 6 kwa unafuu zaidi wa gharama ya data kati ya Nchi 55 Barani Afrika.
INASIKITISHA: MTANZANIA ASIMULIA MISUKO SUKO WANAYOIPITIA NCHINI UKRAINE, MILIO YA MABOMU, UBAGUZI