Jeshi la polisi wilaya ya Nkasi limefika katika Kijiji Cha Mpasa kilichopo Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa na kufukua mwili wa Marehemu Ambaye alikuwa ni Mama mjamzito miezi 7 aliyefariki kwa kipigo Cha mme wake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio Hilo Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Peter Lijualikali amelaani vitendo vya jamii hiyo kuwa na mfumo wa kuficha maovu yanayo endelea Katika Kijiji hicho ambapo amewataka kuondokana na mfumo huo ambao ni hatarishi kwao hasa kwa Mama mjamzito.
Aidha baada ya Jeshi la polisi kufukua mwili huo na uchunguzi kufanyika Dkt Englabeti Kapembwa Ambaye ni Daktari wa Wilaya ya Nkasi akasema kuwa Uchunguzi umeonyesha kuna mashambulio ya kipigo sehemu mbalimbali ya mwili wa marehemu, huku ikionyesha Kizazi (Uterus) kikiwa kimechanika kilichopelekea damu nyingi kuvujia ndani na kusababisha kifo Cha Mama huyo aliyekuwa mjamzito.
WATANZANIA WALIOKWAMA UKRAINE WASIMULIA “USIKU HATUTAKIWI KUWASHA TAA, MILIO YA MABOMU, TUSAIDIENI”