Kwenye story kubwa za Wiki hii kuna hii ya Wamarekani 20 wenye figo moja ambao wamefanikiwa kufika katika kilele cha juu kabisa cha Uhuru, Mlima Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Figo Duniani.
Wageni hao walitumia siku 8 za kawaida kupanda Mlima Kilimanjaro kwa njia ya Lemosho na kushukia Mweka.
Wameiambia dunia kuwa kuchangia figo kwa wagonjwa hakukufanyi kuwa mlemavu huku wakichangisha fedha kusaidia wagonjwa wa figo “Unaweza kuwa na figo moja bado ukabaki kuwa binadamu mkamilifu”
Walisindikizwa na ndugu zao 6 kupanda Mlima Kilimanjaro, wawilj tu wenye figo moja hawakufika kileleni.