Mwandishi wa Habari wa Marekani anayefanya kazi nchini Ukraine ameuawa kwa kupigwa risasi katika mji wa Irpin, nje ya Kyiv, Brent Renaud, mwenye umri wa miaka 50, alikuwa mwandishi wa habari na mtengenezaji wa filamu ambaye alikuwa akifanya kazi katika eneo hilo kwa muda sasa.
Mkuu wa Polisi wa Kyiv Andriy Nebytov amesema Mwandishi huyo amepigwa risasi na Wanajeshi wa Urusi na hiki ni kifo cha kwanza kuripotiwa cha mwandishi wa habari wa kigeni aliyeripoti vita nchini Ukraine.
Waandishi wengine wawili walijeruhiwa na kupelekwa hospitali, Mmoja wa Waandishi waliojeruhiwa, Juan Arredondo, amesema alikuwa na Renaud wakati waliposhambuliwa “Tulikuwa kwenye moja ya madaraja huko Irpin, tukienda kupiga picha za wakimbizi waliokuwa wanaondoka, na tukaingia kwenye gari
“Kuna Mtu alijitolea kutupeleka kwenye daraja lingine na tulivuka kituo cha ukaguzi, kabla ya kuanza kutufyatulia risasi, kwahiyo dereva akageuza, waliendelea kupiga risasi, tulikuwa sisi wawili, Rafiki yangu Brent Renaud, akapigwa risasi, nilishuhudia akipigwa risasi shingoni”