Aliyewahi kuwa rais wa Marekani Barack Obama amekutwa na maambukizi ya corona baada ya kufanyiwa vipimo.
Obama ametangaza kuwa na maambukizi hayo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.
“Nimekutwa na covid. Nimekuwa nikiwashwa kwenye koo kwa siku mbili, lakini ninajisikia vizuri” alisema kwenye akaunti yake rasmi ya Twitter.
Obama pia alieleza kuwa yeye na Mkewe Michelle Obama wameshapata chanjo na Mkewe amepimwa hana maambukizi.
Pia amekumbusha wale ambao hawajapata chanjo kuhakikisha wanachanja licha ya kuwa visa vya maambulkizi vinapungua.