Rais Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania washughulike na masuala ya unyanyasaji kuanzia ngazi za familia ili linapokwenda kitaifa iwe rahisi kulikabili.
Ametaja changamoto kubwa iliyopo katika ngazi ya familia ni watu kuongea wenyewe na kuyamaliza hali inayofanya unyanyasaji kuendelea kwa watu wenye walemavu na wanawake.
Rais amesema hayo jijini Dodoma akiongea na watu wenye ulemavu.