Maelfu ya madaktari, wauguzi na wahudumu wengine katika sekta ya afya nchini Haiti wamefanya mgomo nchini kote kupinga wimbi la utekaji nyara uliokithiri kwa watu wa sekta yao.
Waandamaji katika viunga vya miji kadhaa ya taifa hilo la kisiwa walichoma matairi na kuweka vizuizi katika maeneo ya barabara.Maandamano hayo ya siku tatu yalionza Jumatatu na kutarajiwa kumalizika leo hii yalisababisha kufungwa kwa vituo vya tiba katika jiji la Port-au Prince, na kusalia vitengo vya dharura tu.
Idadi jumla ya watu waliotokwa kwa mwaka uliopita ilifikia 655, ambapo serikali inasema inaweza kuwa kubwa zaidi ya hiyo kwa kuwa visa vingi havijaripotiwa.