“Nawashukuru Wageni wote mliokubali wito wetu karibuni sana, leo March 17 umetimia mwaka mmoja tangu alipotutoka Mpendwa wetu Dr.Magufuli, sisi Wanafamilia tumeiandaa siku ya leo maalum kwa ajili ya misa takatifu ya kumuombea na kuenzi maisha yake”
“Ni imani yangu katika Dini zote tumefundishwa kushukuru kwa kila jambo naomba muungane nami katika kumshukuru Mungu, tunamshukuru Mungu kwa Neema zake kwani ilimpendeza kujifunza mema mengi kutoa kwa Hayati Magufuli hakika tutayaishi na kuyaenzi daima”
“Sisi Wanafamilia inatuwia vigumu kumtaja kila mmoja aliyekuwa nasi tangu msiba wa Hayati Magufuli, tunakushukuru Rais Samia kwa kuwa nasi kwa ukaribu sanasana wakati wote tulipoondokewa na Baba yetu”
“Rais Samia naomba nikiri kukupigia simu lakini kwa bahati mbaya sikufanikiwa ila baadaye ukanipigia nikakupa mwaliko huu ambao uliupokea kwa moyo mkunjufu na ukaahidi kuja ingawa haikuwa kimaandishi nashukuru mno, asante sana kwa kuja licha ya kuwa una majukumu mengi ya Kitaifa na Kimataifa umeniheshimu sana Mama tunakuombea Mungu akupe nguvu ya kuendelea kuongoza Taifa vema na Mungu azidi kukulinda akupe maisha marefu” ——— asema Mama Janeth Magufuli leo Chato Geita.