Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Daglas Kinungunyi Mfanyabiashara na mkazi wa Nyamidaho wilayani kasulu Mkoani Kigoma ameuawa kwa kupigwa risasi na Watu wanaosadakiwa kuwa ni Majambazi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma ACP James Manyama amesema majambazi hao walimvamia wakiwa na bunduki moja aina ya AK 47.
Daglas mwenye umri wa miaka 38 alipigwa risasi katika mkono wa kulia na kwenye nyonga na kusababisha kifo chake ambapo baada ya kutekeleza tukio hilo waliiba fedha ambazo bado kiasi chake hakijajulikana.