China imesema haitotuma silaha wala msaada wa kivita Ukraine wala Urusi bali itapambana ili kumaliza vita hivyo “Tunapinga vikali vita ya Ukraine na Urusi na hatupo tayari kuichochea vita hiyo kwa kukaa upande wowote bali tutafanya kila namna kuvimaliza vita”
Kupitia mahojiano maalum na CBS, Balozi wa China nchini Marekani, Qin Gang amesema China ni sehemu ya kutafuta suluhisho na haitaki kuwa sehemu ya tatizo.
“Rais wa China Xi Jinping aliongea na Putin siku ya pili tu ya vita hiyo na akamuomba Putin afanye mazungumzo ya amani na Ukraine, Putin alisikiliza na akaelewa ndio maana tumeona awamu nne za mazungumzo zikifanyika kati ya Ukraine na Urusi”
Alipoulizwa kwanini China hailaani uvamizi wa kijeshi uliofanywa na Urusi nchini Ukraine, Balozi Qin amejibu “Ni ujinga kufikiri kwamba kulaani kutatua matatizo, tunahitaji Diplomasia nzuri na tutaendelea kupambana kuleta amani sio kulaani”