Maserati imezindua gari lake jipya la Grecale SUV jana tarehe 22 March 2022, ni SUV ya pili tu katika historia ya brand hiyo ya kifahari ya Italia na ni gari lao la kwanza litakalo tumia umeme kwa 100%.
Ni hatua ya mapema kuelekea kufanya brand ya maserati kuwa ya kutumia umeme kikamilifu ifikapo mwaka 2030, wakati huohuo aina zote za Maserati zitapatikana katika matoleo ya umeme kufikia 2025, watendaji wa Maserati walisema.
Grecale pia itapatikana ikiwa na injini ya V6 ya utendaji wa juu au yenye injini ya silinda nne na mfumo wa mseto mdogo, matoleo ya SUV yanayotumia mafuta yatauzwa baadaye mwaka huu, toleo hili jipya, linaloitwa ‘Grecale Folgore’, litaanza kuuzwa 2023, bei za Grecale GT zitaanzia $63,500.
Maserati haikutoa bei kwa matoleo mengine. Matoleo ya Grecale yanayotumia mafuta yatatolewa kwa mauzo baadaye mwaka huu, yakiwa kwa bei ya chini zaidi.