Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye amesema Serikali imetoa zaidi ya bilioni 20 katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa barabara ili kuufungua Mkoa wa Kigoma kwa kuunganisha barabara za lami na Mikoa jirani na kuimarisha usafiri wa ndani ya ziwa Tanganyika, Reli na usafiri wa Anga.