Tanzania Breweries Limited (TBL) yaalika kampuni chipukizi za kiuvumbuzi nchini kujiunga na programu ya Accelerator 100+ na kuwa kwenye nafasi ya kupata dola za kimarekani 100,000
Tanzania Breweries Limited (TBL) inayomilikiwa na kampuni ya AB InBev imetoa wito kwa wavumbuzi kutoka mikoa yote nchini kutuma maombi ya kujiunga na programu ijulikanayo kama 100+ Accelerator ili kuchangia katika kutafuta suluhisho za changamoto za maendeleo endelevu.
Programu ya 100+ Accelerator iliyoanzishwa mwaka 2018 imefanya kazi nyingi ikishirikiana na kampuni kubwa duniani kutafuta suluhisho za changamoto za ugavi, utunzaji maji, kilimo endelevu, mabadiliko ya tabia nchi, ukuaji wa pamoja na viumbe hai.
Mwaka huu programu hii imelenga kutafuta suluhisho za kivumbuzi zitakazokua kwa haraka na kuleta mabadilko makubwa kwenye maeneo yenye changamoto.
Programu ya 100+ Accelerator imekua ikijikita kufanya kazi na kampuni ndogo chipukizi ambazo tayari zilikua na bidhaa sokoni au zinazokaribia kwenda sokoni. Vilevile, programu hii imedhamiria kuwezesha kampuni zinazongoozwa na wajasiriamali wenye shauku na wenye ukaribu na watu wa aina mbalimbali wenye ujuzi na wenye nafasi kubwa ya kufanikiwa.
“Sasa tumeanza rasmi kupokea maombi ya msimu wanne wa Accelerator 100+, programu ya kimataifa kwa udhamini wa AB InBev na mashirika washiriki. Accelerator 100+ inafanya kazi na kampuni chipukizi kupata suluhisho endelevu za changamoto za dunia zinazohusiana na maji, uchumi endelevu, mabadiliko ya tabia nchi, kilimo, ukuaji wa pamoja na viumbe hai. Baada ya kuchaguliwa, washiriki watapata ushauri, mafunzo na kiasi cha pesa dola za kimarekani 100,000 zitakazowasaidia kutekeleza miradi yao ya majaribio kwa kushirikiana na baadhi ya chapa pendwa duniani” alisema Abigail Mutoboyerwa, Meneja wa Masuala Endelevu TBL..
Kwa miaka miwili iliyopita, programu hii imeongezea uwezo kampuni 70 kwenye nchi zaidi ya 20. Programu ya 100+ Accelerator inaongezea uwezo wajasiriamali wenye shauku kwa kuwasaidia kuleta bidhaa zao sokoni haraka. Kampuni hizi zinazochipukia zimefanikisha kuleta zaidi ya dola za kimarekani milioni 300 na zinaendelea kukua kwenye ngazi ya kimatatifa ili kufikia malengo ya programu, kuongeza kasi ya kuipeleka dunia kwenye kutumia suluhisho endelevu na kufanya biashara kwa njia sahihi na si njia rahisi.
“Tumeona kazi iliyofanywa na 100+ Accelerator kusaidia wajasiriamali wenye shauku ya kutafuta suluhisho za changamoto za kimataifa na kusaidia kuleta suluhisho zao sokoni haraka. Ushirikiano huu ni nafasi ya kujumuika pamoja katika kuongeza kasi ya kupata ulimwengu endelevu zaidi wakati kila kampuni ikiendelea kujitahidi kufikia malengo yake ya kuwa endelevu,”alisema Mkurugenzi wa TBL Jose Moran.
Kampuni moja au shirika moja peke yake haiwezi kuleta suluhu ya changamoto ya sasa ya kutafuta suluhisho endelevu na 100+ Accelerator imekuwa mstari wa mbele kujenga ushirikiano na wanasayansi, wavumbuzi, wajasiriamali na kampuni duniani kote katika kutambua na kukuza suluhisho endelevu mpya.
“Pamoja na jamii ya Tanzania, tumekua tunakusanya chakula kilichotupwa na kukibadilisha kuwa chakula cha wanyama na mbolea halisi, vilevile kampeni ya +100 Accelerator imefanya kazi kubwa kuwezesha biashara nyingi kutafuta suluhisho za baadhi ya mambo ya kimazingira yenye uharaka na changamoto za kijamii,” alisema xxxxx Chanzi Limited.
Waombaji wote watafanyiwa tathmini kwa awamu na alama zitatolewa kulingana na:
• Kuendana na changamoto endelevu zilizotambuliwa
• Uwezo wa kuonyesha kuwa bidhaa inafaa sokoni
• Ujuzi wa mauzo na timu ya mauzo
• Uwezo wa kufanya majaribio kwenye eneo lolote duniani litakaloteuilwa
Mchakato wa kuchagua waombaji una hatua mbalimbali, na 100+ Accelerator iko tayari kuwasiliana na kampuni chipukizi kwa kipindi chote. Nafasi za maombi ya awamu ya nne ya programu yatafunguliwa Machi 28, 2022, na kufungwa Aprili 30, 2022. Tuma maombi kupitia https://www.100accelerator.com/.