Kutoka Jamuhuri ya kidemokrasi ya Kongo, mji wa Kinshasa una wakazi zaidi ya milioni kumi sawa na mara mbili ya Dar es salaam ambapo ili kuondoa msongamano na kuepusha zile ajali ndogondogo za mara kwa mara uongozi wa jiji hilo umeamua kuweka aina hii ya taa za barabarani.
Mkuu wa usalama barabarani Vale Manga Wilma amesema aina hii ya taa za Robot imesaidia kupunguza msongamano na kuleta urahisi ambao haukuwepo mwanzoni.
Robot hizi zinatumia umeme wa jua ambapo huwa zinafanya kazi saa 24 huku zikiwa na camera pia ili kurekodi kila tukio ikiwemo mwenendo wa magari.
Robot hizi pia zimewezeshwa kuweza kufanya baadhi ya vitu kama binadamu au kama askari wa usalama barabarani anavyofanya ikiwemo kunyanyua mkono kuongoza magari na kutoa sauti (kuongea) kwenye kuvusha watu.
Kingine kizuri ni kwamba hizi taa zimetengenezwa na Mainjinia wa hapohapo Congo DRC waitwao WITECH ONG.
Unapenda stori kama hizi zisikupite mtu wangu? kazi yangu ni kukuletea kila kitu kinachonifikia, nipo tayari kukutumia wakati wowote zinaponifikia… jiunge na mimi kwenye twitter kwa kubonyeza HAPA, instagram HAPA na facebook HAPA