Mkurugenzi Mtendaji wa Tesla Elon Musk amenunua asilimia 9 za hisa katika mtandao wa Twitter na sasa anakuwa Mwanahisa mkubwa zaidi wa mtandao huo wa kijamii ambao kipindi cha nyuma alihoji jukwaa hilo kuhusu misingi ya uhuru wa kujieleza.
Lengo kuu la ununuzi wa hisa milioni 73.5 wa Musk, wenye thamani ya takriban dola bilioni 3, halijajulikani. Hata hivyo mwishoni mwa mwezi Machi Musk, ambaye ana wafuasi milioni 80 Twitter, alihoji uhuru wa kujieleza kwenye Twitter na kama jukwaa hilo linahujumu demokrasia.
Haijulikani ni lini Musk alinunua hisa. Jalada la Tume ya Usalama na Ubadilishanaji la Marekani liliweka hadharani Jumatatu kuwa tukio hilo lilitokea Machi 14.
Musk pia ameibua hisia tofauti juu ya uwezekano wa kuanzisha mtandao wake wa kijamii ili kuongeza upinzani.