Ripoti kutoka nchini Uganda zinasema Wanawake nchini humo wamefanya maandamano asubuhi hii wakishinikiza Wanaume zao kuwaongezea kiwango cha pesa ya matumizi wanachowaachia asubuhi wanapoondoka nyumbani (Kodi ya Meza au kwa Kiganda Kameeza) wakidai gharama za maisha zimepanda, Wanawake hao pia wamelalamika kuwa Wanaume hawawapi heshima wanayostahili na hawathamini mchango wao kwenye Familia.
Wanawake hao wamesema licha ya gharama za maisha kuwa juu wanasikitika kuona bado Wanaume wanaendelea kuacha pesa ileile ambayo walikuwa wanaacha zamani “Kama Mwanaume alikuwa anakuachia Elfu 10 mwaka jana na leo anataka aache ileile bila ya kuwaza kuwa gharama za maisha zipo juu”
Ayo TV & Millardayo.com imekuandalia taarifa kamili unaweza ukabonyeza play.
ASKOFU GWAJIMA AIBUKA NA HOJA NZITO YA KITAIFA “TUTAPATA RAIS WA AJABU TUTAANGUKIA PUA”