Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima 18.04.2022 amemtembelea binti mwenye umri wa 15 ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili kutokana na mgogoro wa kifamilia alikatishwa masomo na kutakiwa kuozeshwa.
Ambapo ndoa hiyo ilitakiwa kufungwa tarehe 15.04.2022 siku ya ijumaa, viongozi wa mtaa huo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi walifika eneo tukio kuzuia ndoa hiyo na kuwashikilia watuhumiwa wa 3 muoaji, sheikh pamoja na mshenga kwa mahojiano.