Ni Mbunge wa Jimbo la Ulanga na Mfanyabiashara Mhe Salim Alaudin Hasham mbali na kwamba ameendelea kuimarisha sekta mbalimbali katika jimbo lake.
Kwasasa yuko kazini na hapa anazungumza kuhusu mgodi wake ambao umewapatia ajira zaidi ya Vijana 500.
‘Huu ni mgodi ambao unapatikana Mahenge wilayani Ulanga mkoani Morogoro, ambapo kwa mara ya kwanza mgodi huu unaanzishwa tulikuwa na vijana wapatao 100 ambao kipindi hicho tulikuwa na vifaa vidogo sana ila kwasasa Mungu ametujalia kama unavyojua tunagawana riziki kwahiyo tumeongeza vijana takribani 400 kwa nafasi mbalimbali’_ Mbunge wa Ulanga Morogoro Mhe.Salim Alaudin Hasham
‘Mgodi huu unatoa madini mbalimbali, Spinel,Ruby, Safaya na bado shughuli zinaendelea kila jimbo na mengi yanafanyika kuhakikisha Ulanga inabadilika’- Mbunge wa Ulanga Morogoro, Mhe Salim Alaudin Hasham
‘Sio kwamba natoa tu ajira hata juzi juzi mmeshuhudia nimetoa mabati 1190 kwa kaya 119 ambazo ziliezuliwa na upepo mkali na kukosa mahali pakuishi, hivyo nawathamini sana Wananchi wa jimbo langu la Ulanga na kuna mengi yanakuja mazuri huu ni mfano wa mtumishi kuwatumikia Wananchi na kutoa ajira ili waweza kujipatia kipato kitakachoweza kuendesha familia zao’- Mbunge Salim
‘Na pia ningependa kuongezea kuhusu suala la Elimu hususani wanafunzi wote wa Jimbo langu la Ulanga wanaofaulu kuanzia kidato cha nne kwenda cha tano nitawasomesha wote kwa kipindi nitakachokuwa madaraka kuwatumia Wananchi wangu wa Ulanga’- Mbunge
NYUMBA 200 ZILIZOEZULIWA PAA ULANGA, MBUNGE AWAFUTA MACHOZI