NI Mei 4, 2022 ambapo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alipohojiwa kupitia mahojiano maalumu na Azam TV alizungumzia wabunifu wa ndani akiwemo Godfrey Magila.
Godfrey Magila ni Mmiliki wa Kampuni ya Magilatech ambayo inahusika katika utengezaji na ulinzi wa mifumo ya kidigital ,imejikita zaidi kwenye utengezaji wa Mifumo ya Malipo, Mawasiliano na Elimu na kwenye Upande wa Ulinzi wa Mifumo imekuwa ikitoa huduma ya kulinda mifumo kwa kuidukua kabla ya wadukuzi nakuziba njia ndani na nje ya nchi.
Rais akizungumza katika mahojiano hayo alisema dhumuni la Serikali ya Awamu ya Sita ni kuendeleza ndoto za vijana nchini hususani katika masuala ya teknolojia ambapo Serikali itajenga Chuo Kikubwa mkoani Dodoma kitakachotoa mafunzo ya mifumo ya TEHAMA.
‘Tunakusudia sasa kukuza ujuzi wa vijana wawe na ubunifu kupitia ICT, tunapanga kujenga chuo kikubwa hapa Dodoma cha ICT lakini ukiacha chuo tayari Costech, SIDO na wengine wana programu nzuri sana za kukuza vijana“- Rais Samia
“Kuna vijana wametoka wazuri katika hii mifumo yetu chukua mfano kuna kijana anaitwa Magila kutoka Magilatech yeye ameanza na Costech (Atamizi ya Tume ya Science na Technolojia) yuko DRC anatengeneza mifumo ni kijana wa kitanzania”- Rais Samia
Bw.Godfrey Magila mwenye umri wa miaka 30 alianzisha kampuni yake mnamo mwaka 2012 katika Atamizi ya Tume ya Science na Technologia (Costech) ambapo mpaka sasa wameshatoa ajira kwa vijana 125 ndani na nje ya Nchi wakihudumia nchi mbalimbali ikiwemo Congo, Dubai, Zambia na Eswatini.
MTANZANIA MWENYE MIAKA 30 AMILIKI KAMPUNI DUBAI , AJIRI VIJANA 125, MSIGWA ASHANGAZWA
RAIS SAMIA AMZUNGUMZIA KIJANA WA KITANZANIA ANAYEMILIKI KAMPUNI YA TEKNOLOJIA