Ni Mei 10, 2022 ambapo Waziri wa Nishati, January Makamba anatoa kauli ya Serikali kuhusu bei ya Mafuta.
Serikali imetenga Tsh BILIONI 100 ili kukabiliana na changamoto ya upandaji wa bei za mafuta, serikali imetenga fedha hizo zitakazopunguza makali ya kupanda kwa bei ya mafuta na utekelezaji wa fedha hizo unatarajiwa kuanza Juni 1 2022 kwani kwa sasa tayari wafanyabiashara walishaagiza mafuta na kuyalipia hivyo haiwezi kuwa rahisi kupungua.
Kauli hiyo imetolewa bungeni leo na Waziri wa Nishati Januani Makamba wakati akitoa kauli ya Serikali kuhusu kupanda kwa bei za mafuta na hatua zinazochukuliwa kushughulikia suala hilo.