Magavana wa majimbo manne ya nchini Urusi wamejiuzulu jana wakati huu ambao nchi hiyo ikijiandaa kukabiliana na athari za vikwazo vya kiuchumi kutoka katika Nchi za Magharibi, Shirika la habari la REUTERS limeripoti bila kutaja sababu za kujiuzulu kwao.
Majimbo yaliyotajwa kujiuzulu kwa Viongozi hao ni pamoja na Tamsk, Saratov, Kirov na Mari El ambapo tayari uchaguzi wa kuwachagua Magavana wapya umepangwa kufanyika Septemba mwaka huu.
Hatua hii inaelezwa kuwa ni ya kawaida kwa nchi ya Urusi kwani mara kadhaa Magavana wasiopendwa au kuonekana kutiliwa shaka wamekuwa wakiondolewa mara kwa mara na hivyo huachia ofisi kwa njia ya kutangaza kujiuzulu.
Wizara ya uchumi ya Urusi imesema kuwa uchumi wa Urusi utapungua kwa asilimia 8.8% katika mwaka huu 2022 kutokana na vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na nchi za magharibi.