Mmiliki wa gari lililolipuliwa na watuhumiwa wa kundi la Al Shabaab ameachiwa huru baada ya kutozwa faini ya shilingi milioni zaidi ya 18 za Kitanzania.
Ahmed Dugal Ali ameshtakiwa kwa kosa la kuchangia kutekelezwa kwa ugaidi huo kwa kutoa gari lake lililolipuka na kuwaua polisi wawili katika kituo cha pangani Nairobi Aprili 23 2014.
Mbali na kosa hilo pia amekutwa na kosa jingine la kumpa hifadhi mmoja wa washukiwa Mohamed Abass Hassan aliyefariki wakati wa mlipuko ambapo upande wa mashtaka umedai Dugal Ali alimpatia hifadhi mtu aliyefaham vizuri kwamba alikua gaidi katika eneo la Nyayo Estate jijini Nairobi kati ya mwezi March na April 23.
Mtuhumiwa huyo pia alikua anahitajika kulipa shilingi milioni 10 za Kenya kabla ya kuachiliwa akisubiri kusikilizwa kwa kesi yake Julai 1 2014 ambapo Wanaume wengine wawili waliokamatwa ni pamoja na Abdiaziz Bulle Ali na Mohammed Abdukkahi Falir.
Kwa pamoja na Dugal wamaeachiliwa huru baada ya kitengo cha polisi cha ATPU kusema hawana ushahidi wowote dhidi yao na wanaweza kufika Mahakamani kutoa ushahidi huku upande wa mashtaka ukisema Mahakama ina uhuru wa kuamua kuhusiana na swala la kumuachia mtuhumiwa kwa bondi.
Wakili wa mtuhumiwa Mbugua Mureithi aliiambia mahakama kwamba bwana Dugal alijisalimisha kwa polisi baada ya kugundua kwamba gari lake lilikua limehusika kutekeleza mashambulizi.
Wiki mbili zilizopita polisi waliomba nafasi ya kufanya uchunguzi zaidi ambapo mmoja wa maafisa wanaoendesha uchunguzi alikula kiapo na kuwasilisha ushahidi unaomuhusisha Dugal na kundi la Alshabaab akisema mmoja wa waliokufa wakati wa mlipuko ana uhusiano naye.