WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, anatarajia kuwa mgeni katika ufunguzi wa maadhimisho ya saba ya wiki ya utafiti na ubunifu ya chuo kikuu cha Dar es Salaam yatakayofanyika Mei 24 hadi 26 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, mapema Leo, Makamu Mkuu wa Chuo , Profesa William Anangisye amesema maadhimisho hayo yamebebwa na kauli mbiu ya utafiti na ubunifu kwa manufaa ya kijamii nchini Tanzania.
Amesema katika maadhimisho hayo chuo kikiuu kitaonesha miradi mia moja kati ya miradi ya utafiti na ubunifu zaidi ya 300 ambayo ilifanya vyema zaidi.
Ametaja miradi hiyo ni pamoj na miradi wa maabara ya kidijitali, glavu maizi kwa wenye matatizo y kusikia na kuzungumza na mtambo maalumu wa kuyeyusha shaba kwa ajili ya wachimbaji wadogo nchini Tanzania.
“Chuo kikuu cha Dar es Salaam kitatumia fursa ya maadhimisho hayo kujipambanua katika utafiti ambao ni mojawapo ya majukumu yake makuu kwa kuonesha shughuli zake za utafiti ,ubunifu huduma kwa jamii na ubadilishaji maarifa kwa njia ya kutatua chagamoto mbalimbali “ anasema
Aidha anasema katika siku ya kwanza ya ufunguzi kutakuwa na wazunguzaji wakuu wawili ambao mfanyabiahara Seif Ali Seif pamoja na mkurungezi Mkuu wa Superdol limited ambaye atatoa mada kuhusu ushirikiano wa sekta ya uzalishaji n vyuo vya elimu ya juu nchini Tanzania.